MATOKEO YA NGORONGO HEROES VS MOROCCO U-20 MARCH 18-2018
Timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 20 ya Ngorongoro Heroes imeibuka na ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Atlasi ya Morocco leo Jumapili.
Mchezo huo uliomalizika kwa Ngorongoro kuibuka na ushindi ulipigwa leo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikuwa miongoni mwa waliofika uwanjani hapo kuishuhudia timu hiyo ya vijana.
Timu hiyo iliyopo chini ya kocha Ammy Ninje ilipata goli dakika ya 62 lililofungwa na Muhsin Makame kwa njia ya mkwaju wa penalti kisha kuwainua mashabiki waliokuwapo uwanjani hapo.
Ngorongoro Heroes inatarajia kucheza mchezo mwingine wa kirafiki Machi 21 dhidi ya Msumbiji.

No comments