BREAK NEWS

TULL TIME MANCHESTER CITY 2 $ MANCHESTER UNITED 3




Full Time: jose Mourinho kaukumbusha ulimwengu wa soka kwamba bado anaweza kupata matokeo pale inapobidi, leo kawachelewesha Manchester City kutwaa ubingwa wa Ligi kuu ya Uingereza.
Magoli mawili ya kiungo ghali wa Manchester United Paul Pogba na Chris Smalling kuipa ushindi United wa 3-2 dhidi ya City magoli ya City yakifungwa na Vincent Kompany na Ilkay Gundogan.
United wanakuwa timu ya kwanza kuitungua City katika dimba la Etihad msimu huu na hivyo kuifanya City kusubiri mpaka dimba la Wembley dhidi ya Tottenham kutwaa ubingwa.
Pep Guardiola kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya ukocha kuruhusu magoli 3 katika mechi mbili mfululizo , sasa inabidi awainue wachezaji kuelekea mechi ya UEFA dhidi ya Liverpool dimba la Etihad akiwa nyuma kwa 3-0.

No comments