BREAK NEWS

HII HAPA RATIBA 16 BORA AZAM SPORTS FEDERATION CUP (ASFC)



HII HAPA RATIBA 16 BORA AZAM SPORTS FEDERATION CUP (ASFC)
Hatua ya 16 Bora michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) inatarajiwa kuanza leo February 21-2018 kwa mchezo mmoja utakaofanyika kwenye Uwanja wa Saba Saba Njombe katik ya wenyeji, Njombe Mji FC dhidi ya Mbao FC ya Mwanza, kuanzia majira ya saa 16:00 jioni.
V Young
V VS England Mechi nyingine za Kombe la Shirikisho la Azam Sports Federation Cup, zitaendelea Jumamosi February 24-2018, wakati Singida United watakapowakaribisha Polisi Tanzania kwenye Uwanja wa Namfua saa 16:00 jioni.
KMC watawaalika Azam FC saa 19:00 usiku kwenye uwanja wa Azam Complex Chamanzi.
Jumapili ya February 25-2018 Buseresere watakuwa uwanja wa Nyamagana Mwanza saa 14:00 mchana kuumana na Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Majimaji FC ya Ruvuma watakuwa nyumbani kwenye uwanja wa Majimaji kuwakaribisha Young Africans ya Dar es Salaam saa 16:00 jioni.
Bora Bora
Complex Ndanda FC watakuwa ugenini kucheza na JKT Tanzania saa 19:00 usiku Azam Complex Chamazi.
Jumatatu ya Februari 26-2018 zitachezwa mechi mbili kati ya Kiluvya United vs Tanzania Prisons saa 14:00 mchana katika uwanja wa Mabatini.
Na Stand United watawaalika Dodoma FC saa 16:00 jioni kwenye uwanja wa Kambarage Shinyanga.

No comments