kwi aivusha simba kombe la shirikisho afrika
Okwi aivusha simba kombe la shirikisho afrika
Mshambuliaji kutoka nchini Uganda Emmanuel Arnold Okwi ameifungia timu yake ya Simba bao la ushindi katika mchezo wa mkondo wa pili wa hatua ya awali ya michuano ya kombe la shirikisho la soka barani Afrika dhidi ya Gendamarie jana jioni.
Okwi aliifungia Simba bao hilo pekee katika dakika ya 55 kipindi cha pili cha mchezo huo, ambao ulichezwa katika mji wa Djibouti City, na kuifanya Simba isonge mbele kwa jumla ya mabao matano kwa sifuri.
Katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliochezwa jijini Dar es salaam, Simba ilichomoza na ushindi wa mabao manne kwa sifuri.
Hata hivyo mchezo wa jana ulikwenda mapumziko kwa sare ya bila bao huku Gendamarie wakipoteza nafasi moja ya kufunga na Simba wakipoteza tatu ikiwemo ya Okwi aliyekuwa nahodha katika mchezo wa jana.
No comments