BREAK NEWS

Mshambuliaji wa Simba Emanuel Okwi ameivunja rekodi ya Simon Msuva



OKWI AVUNJA REKODI YA MSUVA

JIUNGE NA NIJUZEHABARI.CO.TZ SASA!

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FACEBOOKTWITTER na INSTAGRAM ili kupata habari zote za Michezo na Usajili! Usikose Kudownload APP yetu ya NIJUZEHABARI BOFYA HAPA
Mshambuliaji wa Simba Emanuel Okwi ameivunja rekodi ya Simon Msuva na Abdulrahman Musa baada ya kufikisha magoli 16 kwenye ligi kuu Tanzania bara ikiwa ni mzunguko wa 19 raundi ya pili msimu huu (2017/18).

Msuva na Abdulrahman walifunga magoli 14 kila mmoja na kuibuka wafungaji bora msimu msimu wa 2016-2017.

 Okwi aliifikia rekodi yao kwenye mchezo ambao Simba ilikuwa ugenini kucheza na Mwadui mechi ambayo ilimalizika kwa sare ya 2-2.

Katika mchezo wa leo ambao Simba imeshinda 5-0 dhidi ya Mbao, Okwi amefunga magoli mawili ambayo yamemfanya aivunje rekodi hiyo.

Hadi sasa Okwi bado anaendelea kuongoza kwenye orodha ya wafungaji wa msimu huu akiwa na magoli 16 akifuatiwa na Obrey Chirwa mwenye magoli 11 huku John Bocco akiwa na magoli 10 katika nafasi ya tatu

No comments