NIYONZIMA KUPAA KESHO INDIA
Kiungo fundi wa timu ya Simba, Haruna Niyonzima anatarajia kusafiri kesho kuelekea nchini India kwa ajili ya kupata matibabu ya majeraha yanayo msumbua.
Niyonzima hakuonekana uwanjani muda mrefu sasa kutokana na majeraha hayo akicheza mechi chache za mzunguko wa kwanza wa ligi.
Raia huyo wa Rwanda alitakiwa kusafiri juma lililopita lakini kuna mambo ambayo hayakuwa sawa yaka chelewesha safari hiyo.
Kaimu Makamu wa Rais wa klabu hiyo Idd Kajuna amesema kiungo huyo alikuwa asafiri jana lakini imeahirishwa mpaka kesho.
"Niyonzima anatarajia kuondoka kesho kuelekea India kwa ajili ya matibabu, ilikuwa aondoke jana lakini kuna vitu vilikwamisha," alisema Kajuna.
Tangu ajiunge na Wekundu hao akitokea Yanga mwezi Julai mwaka jana Niyonzima bado hajakata kiu ya mashabiki wa Simba kutokana na majeraha hayo
No comments