BREAK NEWS

Tetesi za soka Ulaya Jumatano 21.02.2018




Chelsea inakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Bayern Munich katika kumsajili kiungo wa kati wa Borussia Dortmund Christian Pulisic. (Mail)
West Ham iko tayari kumpatia David Moyes mkataba wa miaka miwili mwisho wa msimu huu iwapo atawasaidia The Hammers katika ligi ya Uingereza na raia huyo wa Uskochi tayari anatafuta wachezaji wa kuwasajili msimu ujao(Express)
Beki wa Lazio na Uholanzi Stefan de Vrij , 26 yuko tayari kuondoka katika klabu yake na kuelekea Manchester United lakini Everton na Arsenal pia wana hamu ya kumsajili(Mirror).
Mourinho: Man United waliwadhibiti Chelsea
Chelsea waafikiana kumnunua Morata
Mikel atangaza kuihama Chelsea
United pia ina hamu ya kumsajili kiungo wa kati wa Lazio na raia wa Itali Jorginho, 26. (sun) Barcelona imeishinda Manchester United katika kumsajili kiungo wa kati wa Brazil na Gremio mwenye umri wa miaka 21 Arthur (mail).
Kiungo wa kati wa Watford Abdoulaye Doucore ,25, amedai kwamba klabu kubwa za ligi ya Uingereza zinamnyatia huku Arsenal ikiwa ndio lengo lake kubwa kujiunga nayo.(Mirror)
Conte: Sikuwa nawakejeli Manchester United
Conte: Tutailaza Barcelona mechi ya marudio UEFA
Mkufunzi wa zamani wa Watford Marco Silva ndio anayepigiwa upatu kumrithi Alan Pardew iwapo atandoka West Brom(Birmingham Mail)
Crystal Palace imejiandaa kumsaini kipa wa zamani wa Liverpool na Brazil Diego Cavalieri katika uhamisho wa bure(ESPN)
Liverpool inajiandaa kumsajili kinda wa Lyon na Ufaransa mwenye umri wa miaka 18 Mohamed Bahlouli. (France Football via Sun)
Philippe Coutinho alikuwa na wakati mgumu katika kipindi cha saa 24 zilizopita mjini Barcelona baada ya gari lake kuvutwa kwa kuliegesha katika eneo lisilofaa na baadaye nyumba yake ikavunjwa na kuibiwa.

No comments