HII HAPA RATIBA YA LIGI KUU TANZANIA BARA RAUNDI YA 20 WIKI HII
Ligi kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea kesho Jumatano kwa mchezo mmoja unaokamilisha raundi ya 19 kati ya wenyeji Ndanda Fc dhidi ya Mabingwa watetezi Young Africans kwenye uwanja wa Nangwanda- Mtwara kuanzia majira ya saa 16;00 jioni.
Baada ya hapo kesho kukamilika kwa raundi ya 19 mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania Bara, ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena Ijumaa, Jumamosi na Jumapili ya wiki hii kwa jumla ya mechi 7 kuchezwa katika viwanja tofauti.
HII NDIYO RATIBA KAMILI YA RAUNDI YA 20 MZUNGUKO WA PILI LIGI KUU TANZANIA BARA 2017-2018.
IJUMAA YA FEBRUARY 02-2018
Simba Sc vs Stand United saa 16:00 jioni kwenye uwanja wa Uhuru/Taifa-Dar es salaam
JUMAMOSI YA MARCH 03-2018
Jumamosi ya Match 03-2018 itachezwa michezo minne (4) ambayo ni.
Kagera Sugar vs Majimaji Fc saa 16:00 jioni kwenye uwanja wa Kaitaba-Bukoba
Azam Fc vs Singida United saa 19:00 usiku kwenye uwanja wa Azam Complex (Chamanzi)
Njombe Mji vs Ruvu Shooting saa 14:00 kwenye uwanja wa Sabasaba-Njombe
Tanzania Prisons vs Mbao Fc saa 16:00 jioni kwenye uwanja wa Sokoine-Mbeya.
JUMAPILI YA MARCH 04-2018
Jumapili ya March 04 itachezwa michezo mitatu (2) ambayo ni.
Mbeya City vs Mwadui Fc saa 16:00 jioni kwenye uwanja wa Sokoine-Mbeya
Lipuli Fc vs Ndanda Fc saa 16:00 jioni kwenye uwanja wa Samora-Iringa
Na mchezo wa mwisho unaokamilisha raundi ya 20 utakuwa kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya Young Africans.
Mchezo huo umesogezwa mbele na utapangiwa tarehe sahihi, ili kupisha maandalizi ya mechi ya kimataifa kati ya wenyeji Young Africans dhidi ya Townships Rollers.
Mchezo huo utafanyika March 06- 2018 kwenye uwanja wa Taifa ukiwa ni mchezo wa kwanza katika hatua hiyo ambapo mchezo wa marudiano utapigwa March 16 huko Botswana
No comments