Mfaransa aja na mbinu kubeba ndoo
SIMBA bwana, wanasema eti wanaye Emmaneul Okwi, John Bocco, Asante Kwasi na nyota wengine, tena chini tya Kocha Mfaransa, Pierre Lechantre kwanini sasa wasibebe ndoo?
Kaimu Rais wa klabu hiyo, Salim Abdallah ‘Try Again’ amesema kwa nguvu waliyonayo sasa wana uwezo wa kuifunga Yanga katika mchezo wao na kisha kubeba ubingwa wanaousaka tangu mwaka 2012.
Simba iliondoshwa katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika na Al Masry ya mjini hapa kwa faida ya bao la ugenini, baada ya matokeo ya suluhu wiki moja baada ya mchezo wa kwanza jijini Dar es Salaam ulimalizika kwa sare ya 2-2.
Try Again alisema baada ya kuenguliwa kwenye michuano hiyo wamerejesha nguvu zote Ligi Kuu na wana imani ubingwa umewakalia kwenye njia yao.
“Kwa namna tulivyojipanga kama uongozi, nafasi ya kutwaa ubingwa tunayo. Timu inacheza vizuri na kwa nidhamu kubwa.
“Tumefurahishwa na kiwango cha timu kwenye mechi ya marudiano. Kama sio mapungufu machache ya mwamuzi tulikuwa na uwezo wa kushinda. Wachezaji walijituma na walicheza vizuri.
“Kama tutakwenda kwa morali hii tuna uwezo wa kuifunga Yanga kwenye mchezo ujao na tukaendelea kusalia kileleni mpaka tutakapotwaa ubingwa, tuna imani kubwa na timu yetu,” alisema Try Again, aliyekuwa imara kudhibiti fitna za Waarabu kwenye mchezo wao wa marudiano mjini hapa.
Bocco naye
Naye nahodha wa Simba, John Bocco alisema mchezo wao ujao dhidi ya Yanga utakuwa mgumu, lakini wanajipanga kama wachezaji wakifahamu ndio umeshika hatma yao ya ubingwa wa Ligi Kuu.
“Tumecheza vizuri kwenye mechi hizi mbili za kimataifa, tulikuwa na nidhamu na tumejituma muda wote. Hata hivyo, haya ni mashindano mengine na ligi ni nyingine, lakini tuna uwezo wa kufanya vizuri.
“Mechi yetu dhidi ya Yanga huwa inaamuliwa na mambo mengi, haitakuwa nyepesi. Kama unavyofahamu kuwa Yanga nao wanahitaji hizo alama tatu ili kuwa pazuri, itakuwa mechi ngumu,” alisema Bocco. Mechi hiyo ya watani ilipangwa kufanyika Aprili 7, lakini sasa itasubiri kupisha mechi ya kimataifa ya Yanga na timu itakayopangiwa katika Kombe la Shirikisho Afrika
Noti zasepa
Katika hatua nyingine wachezaji wa Simba wamepishana na kitita cha Sh100 milioni walichoahidiwa kama wangeing’oa Al Masry.
Katika mkwanja huo kila mchezaji aliahidiwa Sh5 milioni, lakini kutokana na matokeo ya mchezo huo kumalizika kwa suluhu mabosi wa Simba wamerejesha fungu hilo benki.
Hata hivyo, baadhi ya mabosi wao walikuwa wakipendekeza angalau nyota hao wapewe kifuta machozi.

No comments