PRISONS MAMBO MOTOO YAFANYA KWELI VPL
MAAFANDE wa Prisons wametakata nyumbani baada ya kulinda ushindi wao wa bao 1-0 iliyopata juzi katika pambano lao dhidi ya Mbao na kuchezwa kwa dakika 49 kabla ya jana jioni kumaliziwa dakika 41 zilizosalia matokeo yakiwa kama yalivyo.
Ushindi huo umeifanya Prisons kufikisha pointi 32, mbili pungufu na Singida United baada ya kila timu kucheza mechi 20.
Mechi hiyo ilichezwa kwa siku mbili kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini hapa na kusababisha Uwanja wa Sokoine kujaa maji ambapo awali mechi ilipangwa kumalizwa asubuhi ikashindikana na kupangwa jioni.
Bao lililowapa ushindi huo muhimu Prisons lilifungwa juzi na Mohammed Rashid na kumfanya afikishe mabao nane katika ligi ya msimu huu.
Katika mchezo uliochezwa mapema uwanjani hapo Mbeya City na Mwadui zilishindwa kutambiana kutokana na ubovu wa uwanja ambao sehemu kubwa uliharibiwa na mvua hizo.

No comments