RATIBA YA LEO JUMAPILI LIGI KUU TANZANIA BARA RAUNDI YA 22
RATIBA YA LEO JUMAPILI LIGI KUU TANZANIA BARA RAUNDI YA 22
Ligi Kuu Tanzania Bara raundi ya 22 inatarajiwa kuendelea leo Jumapili ya March 11 kwa mechi tano zitakazopigwa kwenye viwanja tofauti.
Mechi mbili za mzunguko wa 22 zilizokuwa zichezwe leo Machi 11-2018 zimebadilishiwa tarehe.
Mchezo wa Simba dhidi ya Njombe Mji umesogezwa mbele na sasa utapangiwa tarehe nyingine hiyo imekuja baada ya Simba kuomba kusogezwa kwa mchezo huo ili kupata muda wa maandalizi ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Masry utakaochezwa March 17 mwaka huu Mjini Port Said nchini Misri.
Mchezo wa Kagera na Mwadui uliokuwa uchezwe Machi 11-2018 kwenye Uwanja wa Kaitaba sasa utachezwa Jumanne ya March 13-2018 kutokana na kusogezwa kwa mchezo wao dhidi ya Young Africans uliochezwa leo Machi 9-2018 na kupoteza kwa magoli 3-0.
Chelsea V Manchester Untd
Arsenal TV RATIBA KAMILI YA LEO JUMAPILI YA MARCH 11-2018 IKO HIVI
AzamFC vs Mbao FC saa 19:00 usiku kwenye uwanja wa Azam Complex (Chamazi)
Ruvu Shooting vs Mbeya City saa 16:00 jioni kwenye uwanja wa Mabatini-Pwani.
Singida United vs Ndanda saa 16:00 jioni kwenye uwanja wa Namfua-Namfua.
Majimaji vs Lipuli saa 16:00 jioni kqenye uwanja wa Majimaji-Ruvuma.
Tanzania Prisons vs Mtibwa Sugar saa 14:00 mchana kwenyw uwanja wa Sokoine-Mbeya
No comments