HASSAN KESSY KUIKOSA TOWNSHIP ROLLERS ( LIGI YA MABIGWA AFRIKA)
HASSAN KESSY KUIKOSA TOWNSHIP ROLLERS ( LIGI YA MABIGWA AFRIKA)
Beki wa kulia wa Yanga Hassan Ramadhan Kessy ataukosa mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers kutokana na kuwa na kadi mbili za njano
Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh alisema kuwa Kessy hataruhusiwa kucheza mechi hiyo kutokana na kuzuiwa na kanuni.
Alisema Kessy alipata kadi ya kwanza katika mchezo wa marudiano nchini Shelisheli dhidi ya St Luois kisha nyingine dhidi ta Township Rollers ya Botswana jumanne wiki hii.
Hassan Hassan
Mohamed Hassan "Tumeshaambiwa hatuwezi kumtumia Kessy katika mchezo wa marudiano, amefikisha kadi mbili za njano. Wachezaji wengine wako vizuri hakuna mwenye tatizo kama hilo, lakini tuna watu wa kuziba nafasi yake,"
Kukosekana kwa Kessy ni wazi nafasi yake itachukuliwa beki wa nafasi hiyo Juma Abdul ambaye yuko fiti.
Katika mchezo w kwanza uliopigwa hapa nchini Yanga iliambulia kipigo cha magoli 2-1.
kutokana na matokeo ya awali Yanga inaeenda kupamba mlima kwenye mchezo wa marudiano wiki ijayo.
Katika mchezo huo Yanga inahitaji ushindi wowote kuweza kusonga mbele katika hatua inayofuata
No comments