TIZAMA ABALORA KUIKOSA MBAO FC LEO (CHAMAZI)
TIZAMA ABALORA KUIKOSA MBAO FC LEO (CHAMAZI)
Wakati Azam ikijiandaa kukipiga dhidi ya Mbao FC katika mechi ya Ligi Kuu Bara jioni ya leo, Azam Complex, kipa Razak Abalora, ataukosa pia mchezo wa leo.
Abalora alisimamishwa kutokana na makosa ya kumtupia lawama Mwamuzi Jonesia Rukiya, baada ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Simba, uliochezwa Februari 7, 2018 katika uwanja wa taifa.
Adhabu hiyo itadumu mpaka pale suala lake litakapojadiliwa na Kamati ya Nidhamu kuhusiana na makosa yake ya kumlalamikia Mwamuzi kuwa aliwanyima penati walipokutana na Simba.
Mpaka sasa suala lake bado halijatolewa majibu.
Hii itakuwa ni mechi ya pili anakosa baada ya kushindwa kucheza dhidi ya Mwadui FC ambayo Azam ilishinda kwa bao 1-0.
No comments