BREAK NEWS

TIZAMA KAULI YA YANGA BADA YAKUPOTEZA JANA HII HAPA



Jana Jumanne ya March 6 2018 Yanga ilishuka dimbani kucheza mchezo wake wa kwanza wa round ya kwanza michuano ya klabu Bingwa Barani Afrika dhidi ya Township Rollers ya Botswana.
Mchezo huo ulianza majira ya saa 16:30 jioni na ulipigwa kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam, na kushuhudia wenyeji Yanga wakipokea kichapo cha goli 2-1.
Kipigo hicho kinaiweka rehani tiketi yao ya kushiriki michuano ya klabu Bingwa Barani Afrika hatua ya makundi.
Mchezo wa marudiano unatarajiwa kupigwa March 17 mwaka huu Mjini Gaborone- Botswana, katika Mchezo huo Yanga wanaitaji ushindi goli 2-0 au zaidi ya hizo ili kufuzu hatua ya makundi.
Baada ya mchezo kocha msaidizi wa Yanga Shadrack Nsajigwa aliridhia kuongea na waandishi wa habari na hii ndio kauli yake.
“Tumepoteza lakini hiki ni kipindi kimoja na naimani mechi ya ugenini tunaweza tukapata matokeo vile vile, kwa sababu wenyewe wamecheza hapa wamepata matokeo kwa hiyo hata sisi tutarudi tutajiandaa, tutajaribu kurekebisha makosa yetu sababu tumeona kuwa na wao wanafungika pia”.alisema Nsajigwa.

No comments