WAONYWA KUHUDU KIFO CHA AKWELINI SOMA ZAIDI HAPA CHINI
Waonywa kuhusu kifo cha Akwilina
Wito huo umetolewa leo na Mwenyekiti wa Seneti ya TAHLISO, George Mnali wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma kuhusiana na msimamo wa Jumuiya hiyo kuhusu kifo cha mwanafunzi mwenzao huyo.
Mnali amesema kuwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini wanapaswa kuwa watulivu na wavumilivu wakati vyombo vya usalama vikiendelea na uchunguzi wake kuhusiana na kifo hicho kama ambavyo wameendela kuwa watulivu.
Mbali na hilo amevitaka vikundi mbalimbali ambavyo vimejitokeza kuwasemea wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu kuacha mara moja tabia hiyo kwa kuwa chombo pekee cha kuwasemea wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu ni TAHLISO peke yake.
Ameongeza kuwa wamegundua vikundi hivyo vinatumika kisiasa na vina lengo la kuharibu amani ya nchi kwa kuwa vinawataka baadhi ya viongozi kujiuzulu na wakati hata matokeo ya uchunguzi wa tukio hilo bado haujatoka.
Pia amewatupia lawama wanasiasa kwa kushindwa kulinda kauli zao ambazo ndizo zilikuwa chanzo cha tukio hilo.
RECENT POSTS
TOP STORIES
MOST POPULAR
ABOUT US/ ADVERTISE/ JOBS/ TERMS & CONDITIONS/
CONTACT US/ FREQUENTLY ASKED QUESTIONS/ ABOUT US
IPP MEDIA/ EAST AFRICA RADIO/ ITV/ RADIO ONE/
CAPITAL RADIO/ LOKOPROMO/ NETWORK
© 2018 East Africa Television Limited. All Rights Reserved Together Tunawakilisha
SATURDAY , 3RD MAR , 2018 NA MWANDISHI WETU
Jumuiya ya Taasisi za Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) imewataka wanafunzi wote wa vyuo vikuunchini kuwa watulivu wakati serikali ikiendelea na uchunguzi wa kifo cha Akwilina Akwilin aliyeuawa kwa kupigwa risasi Februari 16, mwaka huu.
No comments