BREAK NEWS

YANGA YAZINDUA RASMI HUDUMA YA KIDIGITALI



YANGA YAZINDUA RASMI HUDUMA YA KIDIGITALI

Ifikapo April 01-2018 klabu ya Yanga itaanza rasmi kipindi chake cha televisheni kupitia runinga ya Azam kitakachojulikana kwa jina la 'Yanga TV Show'.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo, Mwakilishi wa Televisheni wa Azam FC Baruani Muhuza amesema kipindi hicho kitakuwa tofauti na vipindi vingine vya klabu kama Simba TV na Azam TV kwa kuwa kitaandaliwa na kuendeshwa na WanaYanga wenyewe.
Awali Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa alisema Yanga imeamua kuja na mfumo huo wa kidigitali ili isogee karibu ya wanachama na mashabiki wake popote walipo.
Mbali na Yanga TV, huduma ya kupata habari mbalimbali za Yanga kupitia ujumbe mfupi kwenye simu za mkononi imezinduliwa.
Huduma hiyo kwa sasa inapatikana kwenye mtandao wa Tigo ambapo ili uweze kujiunga unatuma neno YANGA kwenda 15501.
Gharama ya ujumbe mfupi ni Tsh 100 tu za kitanzania.

No comments