BREAK NEWS

ZIMEBAKI SIKU 3 TU SIMBA KUKIPIGA NA AL MASRY



Baada ya kupewa mapumziko ya siku moja, kikosi cha Simba leo jioni kimeanza maandalizi ya mchezo wake wa kwanza Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Al Masry.
Kikosi hicho kilipewa mapumziko ya siku moja baada ya mchezo wake wa ligi kuu dhidi ya Stand United uliomalizika kwa sare ya 3-3 ijumaa jioni.
Taarifa ya klabu hiyo imeeleza kuwa timu hiyo ipo kambini tayari kwa maandalizi ya mchezo huo ikianza na mazoezi ya jioni leo na itafanya hivyo hadi jumanne jioni kisha jumatano kushuka kwenye uwanja wa taifa kukipiga na Wamisri.
''Kikosi cha Simba kimeingia kambini tayari kujiandaa na mchezo dhidi ya Al Masry utakaochezwa siku ya Jumatano saa 12:00 jioni'', imeeleza sehemu ya taarifa.
Simba imetinga hatua ya kwanza ya michuano hiyo baada ya kushinda kwa jumla ya mbao 5-0 kwenye mchezo wa hatua ya awali dhidi ya timu ya Gendarmerie Nationale FC ya Djibouti.

No comments