BREAK NEWS

Wakenya watawala Paris Marathon



Nairobi. Wakenya Betsy Saina na Paul Lonyangata wametamba katika makala ya 42 ya maashindano ya riadha ya Electric Schneider Paris Marathon, mapema leo, jijini Paris nchini Ufaransa.
Mshindi wa mbio za wanawake, Betsy Saina, mwenye makazi take nchini Marekani, alitumia saa 2.22.55 kuvuka utepe kushinda taji lake la kwanza katika mashindano makubwa.
Mkenya mwengine, Ruth Chengetich alimaliza wa pili, akitumia saa 2.22.59 akifuatiwa na Muethiopia Gulume Chala ambaye alitumia saa 2:23:06.
Kwa upande wa wanaume, Mkenya Paul Lonyangata aliwaongoza wakenya wenzake kumaliza katika nafasi tatu za mwanzo wa mbio hizo. Lonyangata alitumia saa 2:06:25, huku Mathew Kisorio na Ernest Ngeno wakifuatia, wakitumia saa 2:06:36 na 2:06:41 mtawalia.
Wakati huo huo, mapema leo Kenya ilijiandikia medali yake ya pili katika mashindano ya jumuiya ya madola yanayoendelea, katika uwanja wa Carrara, Gold Coast, Australia.
Medali hiyo ilipatikana katia mbio za mita 5000, kupitia kwa mwanariadha Edward Zakayo aliyemaliza katika nafasi ya tatu na kuitwalia Kenya medali ya shaba, akitumia 13:54.06. Haya in mashindano yake ya kwanza makubwa kuiwakilisha Kenya.
Mganda Joshua Cheptegei alinyakua dhahabu huku fedha ikienda kwa Ahmed Mohammed, kutoka nchini Canada.

No comments