Yanga yachomolewa hatua ya robo fainali FA
Yanga yachomolewa hatua ya robo fainali FA
Ushindi huo unawakutanisha Singida United na JKT Tanzania, huku Stand United wakikutana na Mtibwa Sugar.
By mchomonews
In the headlines Yanga yachomolewa hatua ya robo fainali FA
SUNDAY APRIL 1 2018
By mchomonews
Singida. Timu ya Singida United wametinga nusu fainali ya FA baada ya kuifunga Yanga penalti kwa 4-2 katika mchezo uliomalizika dakika 90 kwa sare ya bao 1-1 na kuwalazimu kupigiana matuta.
Ushindi huo unawakutanisha Singida United na JKT Tanzania, huku Stand United wakikutana na Mtibwa Sugar.
Papy Tshishimbi na Gadiel Michael walikosa penalti kwenye mchezo huo jambo ambalo limechangia kwa kikosi hicho cha Yanga kutolewa nje ya mashindano hayo.
Mashabiki waliofurika kwenye Uwanja wa Namfua walilazimika kufuatilia mechi hiyo huku mvua kubwa ikiendelea kunyesha hasa kipindi cha kwanza.
Baadhi ya viongozi wa benchi la ufundi kwa timu zote walilazimika kujifunika viti vya plastiki ili kuendelea kushuhudia pambano hilo ambalo Singida wameibuka kifua mbele.
No comments