ZIFAHAMU TIMU ZILIZOTINGA ROBO FAINALI KOMBE LA FA
Klabu ya Azam FC imetinga Robo Fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya kuichapa KMC mabao 3-1 jana kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Baada ya ushindi huo Azam sasa inaungana na Njombe Mji iliyofuzu Jumatano katika mchezo wa kwanza kwa kuiondosha Mbao Fc ya Mwanza kwa changamoto za Penalti penalti 6-5 kufuatia sare ya 1-1.
FA Cup Live
Live Man United Pamoja na Njombe Mji pia Azam inaungana na Singida United ya mkoani Singida iliyofuzu Jana mapema ikiwa ya pili katika hatua hiyo ya 16 bora baada ya kuichapa Polisi Tanzania mabao 2-0, mchezo uliofanyika kwenye uwanja Wa Namfua Singida.
Leo tunasubiria timu 3 kati ya Majimaji vs Yanga, Buseresere vs Mtibwa Sugar na Ndanda vs JKT Tanzania zitakazoingana na hizo 3 ambazo tayari zimefuzu.
Baada ya kupata nyingine 3 keaho tutasubiria nyingine 2 kati ya Kiluvya United vs Tanzania Prisons na Stand United ya Shinyanga vs Dodoma Fc ya Dodoma, zitazokamilisha timu 8 zinazoenda robo fainali ya michiano hiyo.
No comments