BREAK NEWS

MATOKEO NA MSIMAMO LIGI KUU TANZANIA BARA FEBRUARY 17-2018



MATOKEO NA MSIMAMO LIGI KUU TANZANIA BARA FEBRUARY 17-2018














Ligi kuu Tanzania Bara imeendelea leo ikiwa ni mchezo wa kwanza kwenye raundi ya 19 iliyozikutanisha Lipuli Fc ya Iringa vs Azam Fc ya Dar es salaam.
Mpaka dakika 90 zinaisha Lipuli Fc 0-0 Azam Fc, huu unakuwa mchezo wa pili mfululizo kwa Azam kutoa sare baada ya Kagera raundi ya 18 na leo dhidi ya Lipuli kwenye raundi ya 19.
Baada ya matokeo hayo Azam wanabaki nafasi hiyo hiyo ya 3 wakiwa na alama 35 nyuma ya Simba na Yanga, huku Lipuli wakifikisha alama 20 na kupanda kwa nafasi mbili kutoka nafasi ya 9 hadi ya 7.
Vikosi vilivyoanza leo Lipuli Fc vs Azam Fc.
Azam Fc:Razak Abarola, Swaleh Abdalah, Bruce Kangwa, Yakubu Mohamed, Agrey Moris, Stephan Kingue Mpondo, Joseph Mahundi, Salimin Hoza, Yahya Zayd, Shaban Idd, Iddi Kipagwile
Kikosi cha Akiba:Mwadini Ally, David Mwatika, Abdalah Kheri, Frank Domayo, Ennock Atta Agyei, Mbaraka Yusuph, Benard Arthur
Lipuli Fc:Mohamed Yusuph, Steven Maganga, Emanuel Kichiba, Ally Mtoni , Novart Lufunga, Fred Tangalu, Shaban Zubery Ada, Zawadi Mauya , Adam Salamba, Malimi Busungu, Jamali Mnyate
Kikosi cha Akiba:Agatony Antony, Samuel Mkomola, Dalueshi Saliboko, Nampaka Mussa, Omega seme, Seif Rashid Karihe, Jarome Lambele .
Baada ya mchezo huo mmoja wa raundi ya 19 kumalizika kwa suluhu kati ya Lipuli na Azam, msimamo wa ligi unaonesha Lipuli kupanda kutoka nafasi ya tisa hadi nafasi ya saba.
USISAHAHAU KULIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI ZA MICHEZO, BOFYA LIKE

No comments