Mfaransa Simba hatanii kabisa awa mkali zaidi ya simba pori
SIMBA inakabiliwa na majukumu mawili makubwa sasa ambayo kama haitajipanga vizuri, huenda ikakwama, lakini Kocha Mfaransa wa timu hiyo, Pierre Lechantre, amewatuliza mashabiki wa timu hiyo akiwaambia mambo mazuri zaidi yanakuja.
Kwanza Wekundu wa Msimbazi hao wana kazi kubwa ya kuhakikisha wanaendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara huku pia wakiwa na kibarua kigumu dhidi ya Al Masri ya Misri kwenye raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho barani Afrika na tayari Lechantre ametoa angalizo la kuwakabili Waarabu hao akisema inahitaji akili nyingi, si kama ilivyokuwa kwa Gendarmarie.
Simba imesonga mbele kwenye kombe hilo baada ya kuiondoa Gendarmerie kwa jumla ya mabao 5-0 katika raundi ya awali huku Al Masri ikisonga mbele kwa kuifunga Green Buffalo ya Zambia jumla ya mabao 5-2.
“Al Masry ni timu bora nchini Misri, wanacheza kwa mipango na kwa nafasi, nafikiri mechi tuliyocheza na Gendarmarie si ya kufananisha na tutakayocheza nayo kwani wako tofauti,” alisema Lechantre.
“Gendarmarie iko chini na Al Masry iko juu, hivyo kama tunahitaji ushindi tunatakiwa kupambana na kuonyesha kuwa kiwango cha Simba kinakuwa siku hadi siku,” alisisitiza kocha huyo Mfaransa.
Kuhusu mipango atakayoitumia katika kuwakabili Al Masry, Lechantre alisema kwa sasa anataka kumaliza mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Mbao FC kwanza kisha ndio hesabu za Waarabu zifuate.
“Simba ina malengo makubwa mawili, kwanza ni matokeo mazuri kwenye mechi zetu za Kombe la Shirikisho ambapo tutacheza na Al Masry, pili kupata matokeo mazuri kwenye ligi na kuchukua ubingwa ili tupate nafasi kwa mara nyingine ya kushiriki mashindano makubwa,” aliongeza kusema kocha huyo.
MZIKI WA BOCCO, OKWI
Wakati huo huo mastraika wa Simba; John Bocco na Emmanuel Okwi, wametajwa kuwa ndiyo washambuliaji bora ndani ya kikosi chao kwani kasi yao ya kutupia mabao imekuwa ya kusisimua msimu huu.
Okwi ndiye aliyeifungia Simba bao pekee la ushindi ilipoifunga Gendamerie 1-0 hapa Djibouti juzi Jumanne, lakini Bocco hakucheza kwani ni majeruhi.
Lechantre alisema washambuliaji hao wana maelewano mazuri uwanjani jambo ambalo linawabeba vilivyo msimu huu.
“Kwenye mechi ijayo nafikiria kuwatumia Bocco na Okwi, ndiyo washambuliaji bora kwenye timu yetu kwa sasa,” alisema Lechantre.
Wachezaji hao wamekuwa na maelewano katika uchezaji tangu walipoanza kucheza pamoja mwanzoni mwa msimu huu wakiwa wamefunga mabao 30 katika mashindano yote msimu huu.
Okwi amefunga mabao 14 Ligi Kuu na mawili Kombe la Shirikisho huku Bocco akifunga 10 Ligi Kuu, moja kwenye Kombe la FA, moja Kombe la Mapinduzi na mengine mawili Kombe la Shirikisho.
NDEMLA, KICHUYA
Katika hatua nyingine, Lechantre ameonekana kukoshwa vilivyo na mavitu ya nyota wake wengine wawili; Shiza Kichuya na Said Ndemla, ambao msimu huu wamekuwa hawakosekani kikosi cha kwanza.
Lechantre alisema tangu amejiunga na Simba ni mwezi mmoja sasa na amekuwa akimsoma kila mchezaji kiuwezo na namna anavyoisaidia timu.
“Nimewajaribu wachezaji tofauti na kuchagua wazuri kwa Simba. Nafikiri kwa sasa ndani ya timu wako wazuri na kila mmoja anatakiwa kuonyesha uwezo wake,” alisema Lechantre.
“Kwa sasa nafikiri, Shiza ameonyesha kiwango kizuri na Ndemla pia kwenye
No comments