BREAK NEWS

Mwanafunzi agundua Program inayolisimamisha Gari ikigundua Dereva amelewa



News

Mwanafunzi agundua Program inayolisimamisha Gari ikigundua Dereva amelewa

February 27, 2018
Leo February 27, 2018 nakusogezea stori kumhusu Mwanafunzi Rutikanga Fiston anayesoma katika Chuo cha  Polytechnic Regional Centre (IPRC) kilichopo nchini Rwanda ambaye ametengeneza program ambayo ina uwezo wa kugundua ikiwa dereva amelewa pombe.
Ukiachilia mbali uwezo wa kugundua kuwa dereva amelewa, program hiyo pia ina uwezo wa kulisimamisha gari pale inapogundua dereva kalewa. 
Program hiyo ambayo inawekwa ndani ya gari ina uwezo wa kugundua kiasi cha pombe ambacho dereva amekunywa kutokana na kupima pumzi yake.
Rutikanga anaamini kuwa uvumbuzi huo utasaidia katika kupunguza matukio ya ajali za barabarani zinazosababishwa na madereva walevi. 


No comments