BREAK NEWS

PAMOJA NA KUWAFAHAMU, KOCHA SIMBA ASISITIZA AL MASRY SI WEPESI




Kocha Mkuu wa Simba, Pierre Lechantre amesema anakijua kikosi cha Al Masry cha Misri, lakini akaonya.
Simba itakutana na Al Masry March 06 mwaka huu katika mechi ya kwanza Kombe la Shirikisho, timu zikiandia Dar es Salaam.
Lechantre raia wa Ufaransa amesema timu hiyo si ya kubeza, ngumu na inahitajika maandalizi ya kutosha.
Kocha kuyo amesema: “Hakuna kisichowezekana, tuna kikosi kizuri na tuna uwezo wa kuwatoa. Lakini haiwezi kuwa rahisi.
“Lazima tujiandae vizuri, tufanye kazi kwa uhakika na ninaamini tutafanya vizuri.”
Kocha huyo amewahi kufanya kazi nchini Tunisia na nchi nyingine mbalimbali za Ukanda wa Afrika Kaskazini na barani Asia.

No comments