Baada ya kufikisha hattrick 50, ronaldo abakiza bao tatu pekee kumfikia messi la liga
Baada ya kufikisha hattrick 50, ronaldo abakiza bao tatu pekee kumfikia messi la liga
Nyota wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo, jana amefikisha 'Hat-trick' ya 50 katika maisha yake ya soka.
Hat-trick hiyo ya 50 ameipata baada ya kufunga jumla ya mabao manne, Madrid ikiitwanga Girona kwa idadi ya mabao 6-3.
Katika mchezo huo uliopigwa Santiago Bernabeu, Ronaldo alifunga mabao kwenye dakika za 11, 47, 64 na 90+1 huku mengine yakifunga na Benzema dakika ya 86 pamoja na Vazquez dakika ya 59.
Mbali na kuweka rekodi hiyo, Ronaldo sasa amebakiza mabao matatu pekee kumfikia mpinzani wake, Lionel Messi wa Barcelona aliyefunga mabao 25 kwenye La Liga msimu huu, huku Ronaldo akiwa na 22.
Ronaldo amempita Luis Suarez kwenye nafasi ya pili, ambapo mpaka sasa ana mabao 21.
Msimamo wa Ligi Kuu Spain sasa unaonesha Real Madrid ikiwa nafasi ya tatu kwa kuwa na alama 60 ikiwa imecheza michezo 29, wakati vinara Barcelona wao wana alama 75.
No comments