Kocha Southampton atupiwa virago
Kocha Southampton atupiwa virago
Taarifa za Pellegrino kutupiwa virago zilitolewa juzi usiku, baada ya kuboronga katika michezo ya Ligi Kuu England na kuiweka pabaya Southampton.
In the headlines Kocha Southampton atupiwa virago
WEDNESDAY MARCH 14 2018
London, England. Klabu ya Southampton ‘Watakatifu’ imemtimua kocha Mauricio Pellegrino, baada ya kushindwa kupata mafanikio msimu huu.
Taarifa za Pellegrino kutupiwa virago zilitolewa juzi usiku, baada ya kuboronga katika michezo ya Ligi Kuu England na kuiweka pabaya Southampton.
Kocha aliyefukuzwa Watford, Marco Silva ameingia katika orodha ya makocha wanaotajwa kumrithi Pellegrino. Pia Silva anawindwa na klabu ya Benfica ya Ureno, lakini ameonyesha dhamira ya kubaki katika Ligi Kuu England msimu ujao.
Kocha huyo alikuwemo katika orodha ya makocha waliotakiwa na Southampton mwaka jana, lakini aliamua kutua Watford baada ya kuishusha daraja Hull City.
Southampton yenye maskani St Mary’s, inashika nafasi ya 17 katika msimamo wa Ligi Kuu England ikiwa na pointi 28.
Kocha huyo amefukuzwa baada ya Southampton kupata kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya Newcastle United Jumamosi iliyopita.
Kocha wa timu ya Fulham Slavisa Jokanovic, anatajwa katika orodha ya makocha wanaowindwa Southampton ambayo Machi 31 inatarajiwa kumenyana na West Ham United.
No comments