BREAK NEWS

Zaidi ya Vibanda 600 vimeungua katika Ajali ya moto Mbagala



Zaidi ya Vibanda 600 vimeungua katika Ajali ya moto Mbagala

Habari kutoka Mbagala Charambe leo March 6, 2018 ni kwamba zaidi ya vibanda 600 katika soko la Mkochela, vimeungua wa moto alfajiri ya leo na chanzo cha moto kinasadikiwa kuwa ni hitilafu ya umeme.
Afisa Habari wa Jeshi la Zima Moto Dar es Salaam Peter Mwambene ameeleza kuwa kwa mwaka huu hii ni mara ya pili, mwingine ulitokea mwezi February na kwamba sababu ya moto huu imekuwa ile ile kwa awamu zote mbili.
Mwambene pia ameeleza kuwa sababu ya moto huo kufanya uharibifu mkubwa ni kwamba vibanda vilikuwa vingi na ambavyo viko karibu karibu na ndani vilikuwa vina nguo ambazo zinachochea moto.

No comments