MATOKEO YA YANGA DHIDI YA WALAYTA DICHA LEO (KOMBE LA SHIRIKISHO
MATOKEO YA YANGA DHIDI YA WALAYTA DICHA (KOMBE LA SHIRIKISHO)
Mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano wa mashindano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Yanga dhidi Welayta Dicha FC unaendelea katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, huku Yanga wakiwa mbele kwa goli 1-0.
Mchezo huo umeanza majira ya saa 16:00 jioni, goli la Yanga limefungwa na Raphael Daud Loth katika sekunde ya 45.
Endelea kuwa nasi ili kupata kila kinachoendelea kwenye uwanja wa Taifa-Dar es salaam.
GOOOOO dakika ya 54 Emmanuel Martin anaipatia Yanga goli la 2, baada ya krosi safi ya Yusufu Mhilu, ni dakika ya 56 Yanga 2-0 Dicha.
Dakika ya 62 Yanga 2-0 Walayta Dicha, Dakika ya 66 Yanga 2-0 Walayta Dicha, dakika ya 67 Yanga 2-0 Dicha, dakika ya 70 Yanga 2-0 Dicha.
Dakika ya 71 beki wa Yanga Andrew Vicent Chikupe anatolewa nje baada ya kuonekana ameumia, nafasi yake inachukuliwa na Nadir Haroub.
Dakika ya 76 Yanga wanafanya mabadiliko mengine anatoka Thabani Kamusoko anaingia Patto Ngonyani.
Dakika ya 80 Yanga 2-0 Dicha, dakika ya 82 Yanga 2-0 Dicha, kipa wa Yanga Youthe Rostand yuko chini baada ya kugongana na mshambuliajiwa Dicha Fc ni dakika ya 84 Yanga 2-0 Dicha.
Baada ya kupatiwa matibabu Rostand sasa amerejea na mpira unaendelea ni dakika ya 86 Yanga 2-0 Dicha.
Mshambuliaji wa Yanga Emmanuel Martin anatolewa nje baada ya kuchezewa vibaya na mchezaji wa Dicha.
Dakika ya 87 Martin anarejea, Yanga wanafanya mabadiliko mengine anatoka Raphael Daud nafasi yake inachukuliwa na Juma Mahadhi.
Dakika ya 90 Yanga 2-0 Dicha, dakika 2 za nyongeza Yanga 2-0 Dicha.
Mpira umeisha katika uwanja wa Taifa Dar es salaam, Yanga wanafanikiwa kuanza vema katika mchezo wa kwanza mashindano ya kombe la shirikisho Afrika kwa kupata ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Walayta Dicha kutoka Ethiopia.
Magoli ya Yanga yamefungwa na Raphael Daud Loth Sekunde ya 45 na Emmanuel Martin katika dakika ya 54.
Baada ya ushindi huo Yanga wanaitaji ushindi au sare yoyote kuweza kusonga mbele katika mchezo wa marejeano utakaofanyika April 17 mwaka huu huko Ethiopia.
No comments