SIMBA SC: HABARI NJEMA LEO ALHAMISI APRIL 05-2018
SIMBA SC: HABARI NJEMA LEO ALHAMISI APRIL 05-2018
SIMBA SC: HABARI NJEMA LEO ALHAMISI APRIL 05-2018
Kikosi cha Simba kimefanya mazoezi leo katika uwanja wa Samora mjini Iringa katika maandalizi ya mchezo uajo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar.
Habari njema ni kuwa beki wa kikosi hicho aliyekuwa nje ya dimba kwa muda mrefu, Salim Mbonde amerejea mazoezini baada ya kuumia juzi Jumanne katika mchezo wa ligi kuu, dhidi ya Njombe Mji mchezo ambao Simba waliibuka na ushindi wa magoli 2-0.
Simba iliweka kambi ya muda mjini Iringa katika kujiweka tayari dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa ligi kuu unaofuata.
Mchezo huo unatarajiwa kufanyika Jumatatu ya April 09 mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro kuanzia saa 16:00 jioni.
Katika mchezo wa awali uliofanyika October 15 mwaka jana, mjini Dar es salaam timu hizo zilitoka sare ya kufungana goli 1-1.
No comments