BAADA YA MBWANA SAMATTA KUKOSA VISSA SASA AIBUKIA ALGERIA
BAADA YA MBWANA SAMATTA KUKOSA VISSA SASA AIBUKIA ALGERIA
Pichani ni Balozi wa Tanzania nchini Algeria Omar Yusuf Mzee akimpokea Nahodha wa Timu ya Taifa Taifa Stars, Mbwana Samatta alipowasili jioni ya leo Uwanja wa Ndege wa Algiers tayari kwa mchezo wa kirafiki wa kimataifa Algeria vs Tanzania utakaochezwa Machi 22,2018
Kuelekea kwenye muchezo hiyo kocha mkuu wa Taifa Stars Salum Mayanga amekisuka upya kikosi hicho kwa kuwapunguza wachezaji baadhi kutokana na sababu mbalimbali.
Baada ya kufanya marekebisho hayo hiki ndicho kikosi kipya cha timu ya Tanzania'Taifa Stars' kinachotarajiwa kucheza michezo miwili ya kimataifa kwenye kalenda ya FIFA.
Ambapo mshambuliaji Mtanzania, Rashid Mandawa anayeichezea klabu ya BDF XI ya Botswana,ameongezwa kwenye orodha ya wachezaji wa kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars.
Wachezaji walioitwa hapo mwanzo na sasa wameondolewa ni: Thomas Ulimwengu, Said Ndemla, Farid Mussa, Hamis Abdallah na John Bocco.
Walioongezwa na kufanya idadi ya wachezaji ndani ya kikosi hicho kuwa 21 ni: Himid Mao, Rashid Mandawa pamoja na Shaaban Idd.
Mchezo wa kwanza unatarajiwa kufanyika March 22 mwaka huu Tanzania akiwa ugenini dhidi ya Algeria na mchezo wa pili unatarajiwa kufanyika March 27 mwaka huu Tanzania akiwa nyumbani dhidi DR Congo
KIKOSI KAMILI KINACHOTARAJIWA KUTUMIKA NI
1:Aishi Manula
2:Ramadhan Kabwili
3:Mohammed Abdulraman
4:Shomari Kapombe
5:Hassan Kessy
6:Gadiel Michael
7:Kelvin Yondani
8:Abdi Banda
9:Erasto Nyoni
10:Himid Mao
11:Abdulazizi Makame
12:Ibrahim Ajibu
13:Mohammed Issa
14:Feisar Salum
15:Mudathir Yahya
16:Shiza Kichuya
17:Yahya Zayd
18:Shabani Chilunda
19:Saimon Msuva
20:Rashid Mandawa
21:Mbwana Samatta
No comments